Saturday, April 2, 2016

UUNDAJI VIKUNDI VYA HISA VIJIJINI,NI TATIZO KIPINDI CHA MASIKA

BOFYA HAPA CHINI KUONA MAAJABU YA LEO


WAJUMBE katika Kikao.


Katika kikao chao,Waelimishaji ngazi ya jamii wa Mradi huo,wamesema kipindi cha masika kila mtu hujikita katika kilimo,ambapo Muelimishaji kutoka Kata ya Mwanase,Paschal Leonard,ameeleza kipindi cha robo mwaka kilichopita,wanakijiji hawakuwa tayari kuhudhuria vikao vya uhamasishaji Vikundi vya Hisa.

KATIBU katika Kikao hicho Grace Moshi akisoma taarifa ya tathimini ya shughuli za utekelezaji wa Mradi wa Pesa Kwa Wote kwa robo ya tatu.

MWENYEKITI wa Kikao hicho;Mhela Gulumati.


Aidha Muelimishaji wa Kata ya Majengo;Winifrida Christian,ameeleza suala la Posho,usafiri na mawasiliano limekuwa kikwazo la kuutekeleza mradi huo wa Pesa Kwa Wote(PWK) kwa watenda kazi wake ili kuwafikia wananchi kuwapa hamasa ya kuanzisha vikundi.

MWENYEKITI wa Kikao,Mhela Gulumati akichangia mada.




Hata hivyo Mratibu wa Mradi huo wa PWK,kutoka Shirika la HUHESO FOUNDATION,Wilbart Wanga,amesema wafadhili wa mradi Care International,waliwezesha usafiri wa baiskeli zenye kasoro,wamepanga kuitatua kasoro hiyo pia nyinginezo katika kikao cha mwisho wa mwaka na wafadhili wao.




Kwa upande wake Afisa Mradi wa shirika hilo;Fatuma Shaaban amesema pamoja na changamoto hizo zilizo sambamba na muingiliano wa mashirika mengine ambayo sera zao katika uanzishaji vikundi ni kutoa vifaa bure kwa walengwa,kinyume na shirika lake,lakini wasibweteke bali hawana budi kuhamasisha uanzishaji vikundi kwa bidii.

AFISA Maendeleo Kata ya Ikinda wilayani Kahama,Machota Mongita akichangia mada katika kikao.


Mradi wa Pesa kwa wote,unatekelezwa na Shirika lisilo la Kiserikali la HUHESO FOUNDATION,kwa ufadhili wa CARE INTERNATIONAL kwa kipindi cha miaka minne na umeanza mwaka 2014,huku ukikabiliwa na changamoto kadhaa zinazotishia kutofikiwa malengo ya mradi huo.

AFISA Mtendaji Kata ya Shilela katika Halmashauri ya Msalala,wilayani Kahama,Neema Mapunda akichangia mada.

KUONA VIDEO MPYA BOFYA HAPA CHINI