SIKU mbili baada ya
Serikali ya Marekani kusitisha na
kuvunja uhusiano wake na Serikali ya Tanzania katika mambo yote yanayohusu
miradi ya Mfuko wa Changamoto za Milenia(MCC),kwa kuondoa Dola za Marekani
Milioni 472.8(zaidi ya Sh.Trilioni 1 na Bilioni 20,kundi la watoa misaada 10
kutoka nchi za Magharibi wametangaza kusitisha ufadhili wao kwenye bajeti ya
Serikali ya Tanzania.
MCC ilisema imefikia hatua
hiyo kutokana na kutoridhishwa na mwenendo wa uchaguzi wa marudio Zanzibar
ambao haukushirikisha vyama vyote na kutoridhishwa na matumizi ya Sheria ya
Makosa ya Mtandao ya 2015.
Fedha hizo za MCC zilikuwa
zigharamie miradi ya sekta za umeme nchini na kulifanyia mageuzi Shirika la Umeme(Tanesco).
Mataifa 10 miongoni mwa 14
ya Magharibi yaliyojitoa ni Finland,Ujerumani,Canada,Japan,Norway,Sweden na
mkusanyiko wa mataifa yaliyo ndani ya visiwa kadhaa nchini Uingereza kama
Scotland na Wales.
Tamko la mataifa hayo 10 kujitoa
kuifadhili Tanzania lilitolewa jana halikueleza sababu ya kusitisha ufadhili
huo.
Kujitoa kwa mataifa hayo
katika kuisaidia Bajeti ya Tanzania kutaifanya kupoteza mamilioni ya Dola za
Marekani,hivyo kusababisha baadhi ya miradi kukwama na kuathiri uchumi wa nchi
ambao unatarajia kukua kwa asilimia 7.2 kwa mwaka huu.
Kwa mujibu wa Katibu Mkuu
wa Wizara ya Fedha na Mipango,Dk.Servacius Likwelile,kujitoa kwa wahisani hao
kumeifanya Tanzania kubaki na msaada kutoka Jumuiya ya Ulaya(EU),Benki ya
Dunia(WB),Benki ya Maendeleo ya Afrika(AfDB) na Denmark pekee.
“Idadi ya wadau wa maendeleo
imepungua,lakini sisi bado tuna matarajio makubwa kuona washirika zaidi kuja katika
kuunga mkono bajeti ya taifa,”alieleza Dk.Likwelile.
Kujitoa kwa wahisani ni
pigo jingine kwa Serikali ya Tanzania,kwani karibu theluthi moja ya bajeti ya
Tanzania mwaka uliopita ilitegemea misaada.
Sababu za MCC
Machi 28,MCC ilitoa tamko
la kuelezea kusikitishwa kwake na Tanzania kutochukua hatua katika masuala mawili
muhimu,ikiwamo kutoendelea kutangaza matokeo halisi ya uchaguzi wa Oktoba
25,2015 visiwani Zanzibar na hatimaye kumtangaza mshindi na badala yake
kuendelea na uchaguzi wa upande mmoja uliofanyika Machi20,2016.
Sababu nyingine ni
kutositisha matumizi ya Sheria ya Makosa ya Mtandao(Cyber Crime Act),kwa
kutoifanyia marekebisho ili iendane na ulinzi wa hakiza raia na uhuru wao wa
mawasiliano.
Marekani imebaini Tanzania
imeendelea kuitumia sheria hiyo mbaya kukandamiza uhuru wa wananchi kwa
makusudi.
Marekani imesisitiza kuwa
moja ya vigezo vikuu vya kupata fedha za MCC ni nchi mshirika kuwa na rekodi ya
kuendesha mambo yake kidemokrasia,hasa kufanya chaguzi zilizo huru na za
haki,jambo ambalo Tanzania imeshindwa.
CHANZO:- Tanzania Daima.
KUONA VIDEO MPYA BOFYA HAPA CHINI