RAIS John Magufuli
amedaiwa kutishiwa kuuawa na kondakta wa daladala,Hamimu Seifu(42).
Mtuhumiwa wa tishio hilo
ni mkazi wa Ujiji Mwananyamala,Jijini Dar Es Salaam.
Mtuhumiwa huyo
alipandishwa kizimbani jana saa saba mchana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi
Kisutu,akiwa chini ya ulinzi mkali wa polisi.
Mtuhumiwa huyo,alifikishwa
mahakamani hapo mbele ya Hakimu Mkazi Hellen Liwa na kusomewa shtaka lake na
Wakili wa Serikali Mwandamizi Kenneth Sekwao.
Mbele ya Hakimu Mkazi
Liwa,Wakili Sekwao alidai kuwa Machi 10,mwaka huu katika Baa ya Soweto iliyopo
maeneo ya Makumbusho,Wilaya ya Kinondoni jijini Dar Es Salaam,Seif alitishia
kutaka kumuua Rais Magufuli kwa maneno.
Katika kesi hiyo iliyovuta
hisia za wengi mahakamani hapo,wakili huyo alidai kuwa Seif alitishia kumuua
Rais Magufuli kwa kusema, “Kwa haya mambo anayoyafanya Rais Magufuli,nipo
tayari kumuua kwa kujilipua kwa kujitoa mhanga.”
Hata hivyo,hakuna maelezo
zaidi kwenye hati ya mashtaka ya namna mtuhumiwa alivyojulikana na kukamatwa.
Baada ya kusomewa shtaka
hilo,mshtakiwa huyo alikana kutenda kosa hilo.
Hata hivyo,baada ya
kusomewa shtaka hilo,Wakili Sekwao aliieleza Mahakama kuwa upelelezi wa kesi hiyo
bado unaendelea na kuomba tarehe nyingine ya kutajwa.
Hakimu Liwa alisema
dhamana kwa mshtakiwa iko wazi endapo atatimiza masharti.
Aliyataja masharti hayo
kuwa ni pamoja na kuwa na wadhamini wawili na kila mdhamini anatakiwa kusaini
hati ya dhamana ya shilingi milioni mbili.
Mshtakiwa alishindwa
kutimiza masharti ya dhamana na kurudishwa rumande hadi Aprili 14 mwaka huukesi
yake itakapotajwa tena.
CHANZO:-
Tanzania Daima.