TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI.
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ameahirisha
Shamrashamra za maadhimisho ya siku ya Muungano kwa mwaka huu, ambayo
huadhimishwa kila tarehe 26 ya Mwezi Aprili, na badala yake ameelekeza
kuwa siku hiyo itakuwa ya mapumziko kama kawaida, na watanzania
waiadhimishe wakiwa majumbani kwao ama katika shughuli zao binafsi.
Kufuatia
kuahirishwa kwa shamrashamra hizo, Rais Magufuli ameelekeza kuwa fedha
zilizopangwa kutumika kwa ajili ya kugharamia Vinywaji, Vyakula,
Gwaride, Halaiki, Burudani mbalimbali na Hafla ya usiku ambazo ni zaidi
ya shilingi Bilioni 2, zitumike kuanzisha upanuzi wa barabara ya “Mwanza – Airport” katika eneo linaloanzia Ghana Quaters hadi Uwanja wa Ndege wa Mwanza.
Barabara
hiyo inafanyiwa upanuzi ili kukabiliana na kero ya msongamano mkubwa wa
magari ambao unaathiri shughuli za kila siku za wananchi.
Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Chato
04 April, 2016