MKUU
wa Wilaya ya Songea,Mkoani Ruvuma,Benson Mpesya,ameviagiza vyombo vya usalama kumkamata
mara moja,Padre mmoja wa Kanisa la Romani Katoliki,Jimbo Kuu la Songea ili
afikishwe mbele ya sheria kwa madai ya utapeli.
Mpesya
alitoa maagizo hayo hivi karibuni wakati akizungumza katika mkutano wa hadhara
wa wananchi wa Kata ya Matimila,Halmashauri ya Wilaya ya Songea,baada ya
kumlalamikia kutapeliwa na Padre huyo,zaidi ya Shilingi Milioni Mbili,walizotoa
kwa ajili ya kupatiwa mbolea.
Baadhi
ya wananchi hao,Yustini Komba na Kotrida Komba walimwambia Mkuu huyo wa wilaya
kwamba,Padre huyo wanayemtambua kwa jina moja la Xavery,alifika Kata ya
Matimila na kujitambulisha kwa wananchi kuwa ametokea Jimboni Songea.
Yustini
akiongea kwa jazba alisema wanamfahamu Xavery kwa muda mrefu,hivyo walimuamini
na kuamua kuchanga fedha kwakuwa walikuwa na shida na Mbolea na waliziingiza
pesa hizo kwenye akaunti ya benki moja kama walivyoelekezwa.
Lakini
baada ya hapo,wamekuwa wakimtafuta Padre huyo bila mafanikio na kila
walipofuatilia kwa Paroko wa Parokia ya Matimila aliyekuwa mwenyeji wa Padre
huyo,pia ameshindwa kumpata.
Mkuu
huyo wa Wilaya,Mpesya,aliwaambia wananchi hao kuwa Padre huyo licha ya
kuwatapeli wao,kitendo hicho pia amekifanya maeneo mengine katika wilaya hiyo
na taarifa juu ya utapeli huo zimewasilishwa katika ofisi yake,hivyo kuaagiza
kukamatwa mara moja kisha afikishwe Mahakamani tayari kwa Sheria kushika mkondo
wake.
Juhudi
za kuwapata viongozi wa Parokia za Matimila na Songea ziligonga mwamba baada ya
kuelezwa na wasaidizi wao kuwa walikuwa katika maandalizi ya Sikukuu ya Pasaka.
KUONA VIDEO MPYA BOFYA HAPA CHINI