WAKATI Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Dkt.John Magufuri,akitoa siku 15 kwa Wakuu wa Mikoa kuwa
wameshughulikia ufisadi wa Mishahara hewa,Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Anne Kilango Malecela
ameibuka kwa kuwapatia siku sita kwa Wakurugenzi wa Halmashauri tatu za Ushetu,
Msalala na Kahama zilizopo wilayani Kahama,kumpatia majina ya watumishi hewa.
Rais Magufuli alitoa siku hizo 15,kwa wakuu wa
mikoa kuwa wameshughulikia suala hilo la mishahara hewa katika mikoa yao wakati
akiwaapisha.
Kabla ya kutoa tamko hilo alilotoa
wakati akizungumza na watumishi na madiwani wa halmashauri zote tatu za wilaya
ya Kahama,alifika Kata ya Mwakata kuwapa pole waathirika wa mvua kubwa ya mawe,iliyotokea
Machi 4, mwaka jana na kusababisha maafa makubwa, ikiwa ni pamoja na kusababisha
vifo vya watu 47 na kujeruhi wengine zaidi ya 90.
Katika ziara yake hiyo ya siku moja
iliyomuwezesha pia kushuhudia baadhi ya miradi ya maendeleo,Kilango alisema
lundo la watumishi hewa katika halmashauri hizo halikubaliki, hivyo ni wajibu
wa wakurugenzi kuhakikisha kuwa majina yao yanawakilishwa ofisi ya mkuu wa mkoa
sambamba na maelezo ya kumbukumbu zao za ajira, wanavyolipwa na kiasi
wanacholipwa.
“Hata wakurugenzi wakiwaficha, tayari orodha yao
ninayo mezani…naomba mniletee majina,”
alisema mkuu huyo wa mkoa aliyeanza kazi hivi karibuni baada ya kuteuliwa na
Rais John Magufuli.
Katika Awamu iliyopita ya utawala wa
Rais Jakaya Kikwete, Anne Kilango alikuwa Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya
Ufundi.
Pia aliwataka viongozi wa
halmashauri hizo kuhakikisha wanaongeza kasi ya kukusanya mapato, ikiwa ni
sambamba na kuongeza weledi ili mapato hayo yasipotee.
“Maendeleo ya Kahama yanatuhusu wote. Sipendi
kumsimamisha mtu kazi kwa tuhuma za ubadhirifu, lakini ikibidi kufanya hivyo
nitafanya kulingana na kasi ya uongozi wa Serikali ya Awamu Tano chini ya
uongozi wa Rais John Magufuli,” alisema.
KUONA VIDEO MPYA BOFYA HAPA CHINI