RAIS wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania,Dkt John Pombe Magufuli,ameliagiza Shirika la Ugavi wa Umeme
Nchini(TANESCO)kuhakikisha linajenga mitambo yake ya kufua nishati hiyo na
kuondokana na tabia ya kukodi ili kumudu kutoa huduma hiyo kwa uhakika na bei
nafuu kwa wananchi.
Agizo hilo alilitoa jana
alipokuwa akiweka jiwe la msingi la ujenzi katika kituo cha kufua umeme cha
Kinyerezi namba mbili Jijini Dar Es Salaam,ambapo alilipiga marufuku shirika hilo la
ugavi,kuhakikisha haliingii Mkataba tena na Kampuni yoyote kwa kukodisha
mitambo ya kufua nishati hiyo.
RAIS Dkt.John Magufuli na Balozi wa Japan Nchini,Masaharu Yoshida,wakikata utepe. |
Rais Magufuli alisema
Tanzania imechezewa vya kutosha hivyo anaona wakati muafaka umefika wa kuachana
na miradi ya kukodi mitambo ya umeme,bali kinachotakiwa ni kujenga ili kuleta
unafuu wa huduma hiyo kwa wananchi.
“Ni matumaini yangu
sintasikia tena mnaleta mapendekezo kwamba tunataka kuongeza mkataba huu au
tunataka kukodi mtambo huu.Suala la kukodi life likafe kabisa,sasa tuwe na
mawazo ya kujenga mitambo yetu,”alisema Rais Magufuli.
Akielezea mradi huo
Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO,Mhandisi Felchesmi Mramba,alisema mradi huo
utagharimu Dola za Kimarekani Milioni 344 na utakamilika baada ya miaka miwili
na utakuwa na mitambo sita itakayofua kiasi cha megawati 160.
“…zitakazotokana na gesi
na mitambo miwili ya mvuke itakayoongeza megawati 80 hivyo kufanya kituo hiki
cha Kinyerezi kuzalisha megawati 240,”alisema Mramba.
Nae Balozi wa Japan nchini,
ambao ndio wanafadhili Mradi huo, Masaharu Yoshida, alisema ujenzi wa mtambo
huo ni muendelezo wa miradi mingi na mizuri baina ya Tanzania na nchi yake
ambayo italeta tija kwa wananchi.
RAIS Dkt.John Magufuli akikagua ujenzi wa Kinyerezi namba mbili. |
Kuanza kwa ujenzi wa
mitambo ya kuzalisha umeme huo,kunafuatia juhudi zilizofanywa na serikali ya
awamu ya tano ya kufanikisha upatikanaji wa Shilingi Bilioni 120,ikiwa ni
asilimia 15 ya fedha zilizopaswa kutolewa na Tanzania na fedha nyingine
Shilingi Bilioni 292 zimetolewa na Japan.
Mradi huo umetanguliwa na
wa Kinyerezi namba moja ambao una uwezo wa kuzalisha Megawati 150 za Umeme,na
mitambo yake tayari imeanza uzalishaji
wa megawati 105 zilizoingizwa Gridi ya Taifa.
KUONA VIDEO MPYA BOFYA HAPA CHINI