KIJANA aliyejulikana kwa jina la Dotto
Paul Shija(21) mkazi wa Uzogore katika manispaa ya Shinyanga ameuawa kwa
kupigwa kitu chenye ncha kali kichwani kisha kuvunjwa mguu wake wake wa
kulia siku ya mkesha wa pasaka baada ya kutoka disko.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa kaimu
kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga Dismas Kisusi alisema marehemu
alifariki dunia Machi 27,2016 saa 4:10 asubuhi katika hospitali ya rufaa
ya mkoa wa Shinyanga.
Akielezea tukio hilo kamanda Kisusi
alisema Dotto Paul Shija alijeruhiwa kwa kupigwa na kitu chenye ncha
kali kichwani na kuvunjwa mguu wake wa kulia katika eneo la Ndembezi
Mbalaji katika manispaa ya Shinyanga na watu wasiojulikana.
Alisema awali marehemu alikuwa disko maarufu kwa jina la Mwanamindi iliyokuwa inafanyika katika eneo hilo.
“Ilipofika majira ya saa tisa
usiku,marehemu alimuaga rafiki yake aliyekuwa naye Joseph Ajusta(21)
mkazi wa Ibadakuli kuwa anakwenda nyumbani kulala,wakati anakwenda
nyumbani aliongozana na Emmanuel Hamis(19) mkazi wa Ibadakuli”,alieleza
Kamanda Kisusi.
“Palipopambazuka marehemu alikutwa eneo
la relini Ndembezi akiwa anavuja damu,akakimbizwa katika hospitali ya
rufaa ya mkoa wa Shinyanga kwa ajili ya matibabu lakini ilipofika saa
4:10 asubuhi akafariki dunia”,aliongeza kamanda Kisusi.
Hata hivyo alisema tayari jeshi la
polisi mkoa wa Shinyanga linamshikilia Emmanuel Hamis aliyeongozana na
marehemu kwa mahojiano zaidi.
CHANZO CHA HABARI-Malunde1 blog
Monday, March 28, 2016
AUAWA AKITOKA MKESHA WA DISCO LA PASAKA
BOFYA HAPA CHINI KUONA MAAJABU YA LEO