TAARIFA KWA UMMA
UAMUZI WA BODI YA WAKURUGENZI YA MCC WA KUSITISHA MAHUSIANO NA TANZANIA YATAWAUMIZA WANANCHI WA VIJIJINI
CHAMA
cha ACT-Wazalendo kimeupokea kwa masikitiko makubwa uamuzi wa Bodi ya
Wakurugenzi wa wa MCC wa kusisitisha mahusiano na Tanzania.
MCC
ni Shirika la misaada la Marekani lilianzishwa na Bunge la Nchi hiyo
mwaka 2004 kwa lengo la kusaidia miradi ya maendeleo katika nchi
mbalimbali duniani kwa ajili ya kuchochea ukuaji wa haraka wa uchumi.
Tangu
kuanzishwa kwake, shirika hili limesaidia miradi mingi ya maendeleo
nchini ikiwemo ujenzi wa barabarani na usambazaji wa umeme vijijini kwa
sasa miradi ya aina hiyo inaendelea sehemu mbali mbali hapa nchini na
miongoni mwao ni pamoja na mradi wa REA,miradi ya barabara kama ile ya
Tnduma Sumbawanga pamoja na Tanga katika barabara ya Horohoro.
Pamoja
na vigezo vingine, kigezo mama kwa nchi kufuzu kupata misaada ya MCC ni
kwa nchi husika kuzingatia misingi kidemokrasia ikiwemo kufanya
uchaguzi ulio huru na haki.
Jana
tarehe 28 Machi 2016 Shirika la MCC lilitangaza kusitisha mahusiano na
Tanzania kutokana na serikali ya Chama cha Mapinduzi (CCM),kubariki
kufutwa kwa matokeo ya uchaguzi wa Zanzibar uliofanyika tarehe 25 Oktoba
205 na kubariki kurudiwa kwa uchaguzi huo tarehe 20 Machi 2016 katika
mazingira ambayo hayakuzingatia misingi ya demokrasia ya vyama vingi na
kuvunja matunda ya mwafaka wa kisiasa na kikatiba uliojengwa kwa gharama
kubwa visiwani humo.
Chama
cha ACT-Wazalendo kinapigania nchi yetu kujitegemea kiuchumi kama
msingi wa kujenga utu na uhuru endelevu wa kisiasa na kijamii. Hata
hivyo tunatambua kwamba katika kipindi hiki nchi yetu inahitaji
mahusiano mema na Jumuiya ya Kimataifa na wadau mbalimbali wa maendeleo
duniani, likiwemo shirika la MCC, katika kuendeleza miradi ya maendeleo.
Shirika la MCC limekuwa mdau mkubwa katika miradi ya barabara na
kusambaza umeme vijini.
Uamuzi huu wa Bodi ya Wakurugenzi wa MCC utawaumiza na kukwaza juhudi za wananchi wa vijijini katika kujikwamua na umaskini.
Tunasikitika
kwamba ubabe wa Serikali ya CCM na woga wake wa kushindana kidemokrasia
umesababisha nchi yetu ikose pesa za MCC ambazo zingesukuma mbele
juhudi za kupambana na umaskini.
Tunatoa
wito tena kwa Serikali ya chama cha Mapinduzi kuacha ubabe na kufifisha
juhudi za miaka ishirini za ujenzi wa demokrasia hapa nchini. Tunatoa
wito maalumu kwa wadau wote wa siasa visiwani Zanzibar kurudi mezani na
kutatua mgogoro wa kisiasa kwa njia za kistaraabu na katika hali ambayo
itarudisha heshima ya nchi yetu katika kukuza demokrasia nchini.
Imetolewa na
Theopister Kumwenda
Makamu Mwenyekiti, Kamati ya Katiba, Sheria na Mambo ya Nje
29/03/2016
KUONA VIDEO MPYA BOFYA HAPA CHINI