VIJANA wanaofanya biashara ya kusafirisha abiria kwa kutumia pikipiki almaarufu;Bodaboda,wameshindwa kudhibiti hasira zao na kuchukua sheria mkononi baada ya kubaini wanafanyiwa Utapeli,na watu waliokuwa wakifanya shughuli za askari wa usalama barabarani kinyume cha sheria huku wakijipatia fedha.
Madereva hao wa Bodaboda hizo,hawakuwa na simile baada ya kubaini mchezo huo mchafu uliikokuwa ukifanya na Watu wawili
waliokuwa wakidai kuwa ni Askari wa Usalama barabarani,ndipo walipowavamia na kuwajeruhi
vibaya baada ya kuwababatiza wakiendeleza hila ya kutekeleza jukumu la ukamataji wa pikipiki zisizo na leseni.
Tukio hilo limetokea
katika kijiji cha Katunguru kata ya Katunguru wilayani Sengerema wakati
watu hao ambao hawakuweza kujulikana majina yao walijeruhiwa sehemu
mbalimbali za miili yao, baada ya kuanza kukamata pikipiki pasipo kuwa
na vitambulisho vya kazi pamoja na kutovaa sare za Jeshi la Polisi
kitengo cha usalama barabarani.
Wameongeza kuwa
baada ya kuwashambulia watu hao kwa kuwadhania kuwa wezi wa pikipiki,
walikili kuwa wao sio maaskari wa Jeshi la Polisi kitengo cha usalama
barabarani wala hawahusiani na jeshi la polis lakini walikuwa wakitumiwa
na Jeshi la Polisi kituo cha katunguru kukamata pikipiki.
Madereva hao
waliliomba Jeshi la Polisi kitengo cha usalama barabarani kuhakikisha
shughuli za ukamataji wa pikipiki zina simamiwa na maaskari wenye weledi
wa kazi hiyo ilikuepuka mataperi wa pikipiki ambao wamekuwa wakitumia
nafasi ya Jeshi la Polisi kuiba pikipiki hususani kwa madereva pikipiki.
Kwa upande wake
Kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi alipohojiwa alisema Ofisi
yake haija pokea taarifa za tukio hilo na kuahidi kufuatilia tukio
hilo.
KUONA VIDEO MPYA BOFYA HAPA CHINI