Monday, June 12, 2017

ACACIA INAFANYA KAZI KINYEMELA NCHINI,INACHOSAFIRISHA SI MAKINIKIA.

BOFYA HAPA CHINI KUONA MAAJABU YA LEO



KAMATI ya pili iliyoundwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt.John Pombe Magufuli,kuchunguza mchanga wa dhahabu unaosafirishwa nje ya nchi,imewasilisha Taarifa yake kwa
kubainisha kilichosafirishwa si mchanga bali ni madini anuai.

Kamati hiyo iliyokuwa na wabobezi wa masuala ya Uchumi na Sheria,pia imebaini kuwa kampuni ya ACACIA Mining Plc inayojishughulisha na uchimbaji na kusafirisha kilichoelezwa Mchanga wa dhahabu ( Makinikia )haina kibali na inafanya kazi kinyume cha sheria.

Mwenyekiti wa Kamati hiyo,Profesa Nehemiah Osoro akiwasilisha taarifa yao,amesema Kamati yake imebaini kuwa kilichokuwa kikisafirishwa na Acacia,hakikuwa mchanga wa dhahabu,bali ni mkusanyiko wa madini zaidi ya kumi ambayo yangeliingizia Taifa pato.

Profesa Osoro amesema pia Kamati yake imebaini kwamba Kampuni hiyo ya Acacia haina uhalali wa kufanya shughuli zake hapa nchini  na imetenda makosa yakiwemo kujipatia mali kwa udanganyifu, uhujumu uchumi, jinai na kuitia hasara taifa.

Aidha Kamati ya Prof. Osoro imebaini kwamba  Makinikia yaliyouzwa nje ya nchi hayakuwa makinikia hasa, bali yalikuwa ni madini mbalimbali huku ikiongeza kwamba  katika mikataba ya uuzwaji wa makinikia hayo, serikali haikuwa sehemu ya mikataba hiyo.

Prof. Osoro ameongeza kwamba jumla ya mapato yote ambayo serikali imepoteza ni Tsh. trilion 68.6 sawa na bajeti ya miaka miwili ya nchi kodi ya mapato ambayo taifa imepoteza ni Tsh. tril 55.07, mrahaba tril 11, bandari tril 1.6. na kwamba jumla ya thamani ya madini kwenye makontena yote 44,277 tangu mwaka 1998 ni Tsh. tril 132.56.

Pamoja na hayo imebainika kuwa uongezwaji wa leseni kinyume cha sheria ambapo imedaiwa kuwa aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini  William Ngeleja na Sospeter Muhongo ndio waliohusika na uongezaji wa muda kwenye uchimbaji wa madini.

Kamati hiyo imetoa mapendekezo Ishirini ambayo Rais Magufuli ameyaridhia ikiwepo kuchukua sheria juu ya kampuni ya ACACIA iliyopo nchini kinyume cha sheria kupitia msajili wa makampuni,sambamba na sheria za madini kuwasilishwa Bungeni na kujadiliwa.

Pia Mawaziri na watendaji wote wa serikali walioshiriki kwa namna moja au nyingine juu ya mikataba ya uchimbaji madini,wachukuliwe hatua za kisheria huku ikiitaka Serikali iwe inafanya ukaguzi wa mara kwa mara kwenye makampuni ya madini.

KUONA VIDEO MPYA BOFYA HAPA CHINI