aidi ya wananchi 40,600 katika visiwa
10 vilivyopo wilayani Ukerewe,wanaokabiliwa na changamoto ya ukosefu wa
umeme kufuatia miundombinu kutokuwa rafiki, wanatarajia kuondokana na adha hiyo.
umeme kufuatia miundombinu kutokuwa rafiki, wanatarajia kuondokana na adha hiyo.
Serikali kupitia Mwekezaji;Rex Energy imejipanga
kutoa huduma hiyo ya umeme,wa nishati ya jua chini ya uangalizi wa Rural
Energy Agency (REA) ikiwa ni kuhakikisha wanajamii wanaishi katika mazingira
salama,anaandika Tunu Herman,aliyekuwa wilayani Ukerewe.
Mkurugenzi mtendaji wa Kampuni ya Rex
Energy,Mhandisi Francis Kibhisa,amewahakikishia wakazi wa visiwa hivyo kumi,kuondokana
na adha hiyo kwakuwa wako tayari kuihudumia jamii.
Akizungumza katika hafla fupi ya uzinduzi wa
mpango huo ulioambatana na utiaji saini mkataba wa ujenzi wa miundombinu ya
nishati ya umeme wa jua katika visiwa hivyo,baina ya Serikali kupitia
Halmashauri ya wilaya ya Ukerewe na Mwekezaji,kwa kuwataka wananchi kuwa na
imani,kwakuwa wamedhamiria kuiondoa changamoto hiyo.
Amesema,“Wananchi waishio katika
visiwa mbalimbali hapa nchini wamekuwa wakipata shida ya kuishi gizani kufuatia
kukosa umeme,huku serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais John Magufuli,
ambayo inaitaka Tanzania iwe ya Viwanda.”
“….. sisi Rex Energy kama
wazalenzo tumeamua kuwekeza katika sekta ya nishati ya umeme wa jua ambao
utakuwa ni rahisi kuwafikia wanachi wengi walio katika maaeneo korofi ikiwa na
kumudu gharama za utumiaji ili kuweza kukuza uchumi kwa wananchi ikiwa na
kujishugulisha na shughuli mbalimbali za kimaendeleo,”alisema Kibhisa.
Ujenzi huo wa mradi katika visiwa 10
umegawanyika katika awamu mbili ambapo visiwa vya Ghana,Bwiro,Kamasi,Burubi
ambavyo tayari viko katika awamu ya kwanza na viko katika hatua ya
kukamilika na gharama yake ni Bilioni 6.4.
Amefafanua kuwa visiwa vya Kweru
kuu,Kweru Mto,Izinga,Zeru,Bushengele na Sizu vitakamilika katika awamu ya pili
na gharama yake ni Bilioni 14.6.
Aidha Kibhisa alisema wakati
wakiendelea na shughuli hiyo watajikita katika masuala makuu matatu amabayo
yako ndani ya jamii ikiwa ni kuboresha mazingira ya shule,ujenzi wa Zahanati na
Visima vya maji salama katika visiwa hivyo ,ili kuweza kwenda sambamba na maendeleo
ya sehemu husika.
Mkazi wa kisiwa cha Ghana, Tatu
Nyerere,akizungumza kwa niaba ya wananchi wanaoishi katika visiwa hivyo alisema,
wanakabiliwa na changamoto za ukosefu wa vituo vya Afya vinavyopelekea adha
kubwa kwa wamama wajawazito kujifunglia njiani ikiwa na kupoteza maisha.
“Tunaishukuru serikali ya awamu ya
tano kwa kutuletea wawekezaji wazalendo ambao wanafahamu wananchi wamaeneo
mengi wanahitaji nini, leo tumempata Rex Enegy amabaye ametuletea umeme,atatujengea
vituo vya afya kuboresha shule na visima vya maji salama,”
“……kwakeli tunamshukuru maana tulikuwa
tunaishi katika maisha hatarishi ya kukumbwa na vifo vinavyoweza kuepukika,magonjwa
ya milipuko tunaamini hata suala la ulinzi na usalama litakuwa lipo katika
visiwa husika,”alisema Tatu.
Naye mkurugenzi wa halmashauri hiyo,Frank
Bahati, alisema wilaya hiyo inakabiliwa na changamoto ya miundombinu kutokana
na Jiogorafia ya eneo hilo kuwa mbalimbali,hali inayochangia kuchelewa kwa maendeleo
hivyo kuishukuru Rex Energy kwa kuamua kutatua
changamoto zilizopo ndani ya jamii ya Ukerewe.