Thursday, April 20, 2017

UPINZANI ZIMBABWE WAUNGANA KUMNG'OA MUGABE

BOFYA HAPA CHINI KUONA MAAJABU YA LEO

VYAMA vikubwa vya Upinzani Nchini Zimbabwe,vimeafikiana kuwa na umoja wenye lengo la kuhakikisha vinakibwaga chama kikongwe cha nchi hiyo kwa kuchukua dola.
 
Vikiwakilishwa na viongozi wao wakuu,vyama vya upinzani nchini Zimbabwe wamekubaliana kuunda umoja kuwania urais kwenye uchaguzi mkuu ujao nchini humo.

Kiongozi wa Movement for Democratic, Morgan Tsvangirai na aliyekuwa makamu wa rais wa nchi hiyo Joice Mujuru wa National people's Party walitia saini makubaliano hayo siku ya Jumatano.

Rais wa nchi hiyo Robert Mugabe awali alitoa maneno ya dhihaka kutokana na mipango ya upinzani aliyodai kuungana kumuondoa madarakani.

Morgan Tsvangirai na Joice Mujuru wameonekana kumaliza baadhi ya tofauti zao.Tsvangirai anasema makubaliano yaliyotiwa saini baina ya vyama viwili ni msingi kuelekea kuunda umoja wa vyama kwa ajili ya kupambana na chama tawala Zanu PF.

Changamoto iliyopo hivi sasa ni kuamua nani kati ya hao wawili ataongoza muungano huo.

Tayari, vyama vingi vidogo vya upinzani vimemuidhinisha Morgan Tsvangirai kuwa mgombea wao wa urais.

Kiongozi wa miaka mingi madarakani Robert Mugabe , alieleza kuwa upinzani umejaa watu wasio na kitu vichwani.

Amesema hakosi usingizi kwa kile kinachoitwa umoja wa wapinzani.

Chanzo: BBC

KUONA VIDEO MPYA BOFYA HAPA CHINI