Tuesday, April 11, 2017

NKAMIA ASHANGAZWA SERIKALI KUANDAA MKUTANO WA ROMA

BOFYA HAPA CHINI KUONA MAAJABU YA LEO

MBUNGE wa Jimbo la Chemba,Juma Nkamia,ameshangazwa kwa kitendo cha Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo,Dr. Harrison Mwakyembe, kuhudhuria Mkutano wa Msanii aliyetekwa,Roma Mkatoliki.
 
Nkamia akichangia maoni kuhusu mapitio ya mapato na matumizi ya fedha za ofisi ya Waziri mkuu na ofisi ya bunge kwa mwaka wa fedha 2017/2018,katika Mkutano wa Bunge,mjini Dodoma,amedai hakuona mantiki ya Waziri huyo kuhudhuria mkutano huo.  .

Amedai na kitendo cha Waziri wa Habari, utamaduni, sanaa na michezo kwenda katika mkutano wa msanii Roma mkatoliki alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari Dar es salaam jana,huku msema chochote akiwa afisa wa Serikali,Zamaradi Kawawa.

Amesema: Jana nilipata nafasi ya kuangalia Press Conference ya Roma. Najiuliza, Waziri wa habari alienda kufanya nini? Akiambiwa ndo alimteka Roma atakataa?

"Mtu alitekwa, serikali ndo inamwandalia press conference na kuisimamia? Ivi kesho mkiambiwa ndo mlihusika kumteka mtakataa? Najua ukweli unauma, lakini lazima tuseme.

"Serikali wakati mwingine mnaingia kwenye mitego wenyewe na mnamgombanisha Rais na wananchi.

"Nimesema ukweli, wengine wataanza kuwaza labda ni kwa sababu nilikosa uwaziri.....No, lazima tuseme ukweli."

KUONA VIDEO MPYA BOFYA HAPA CHINI