AFISA
wa Jeshi la Zimamoto na Uokaji Wilaya ya Kahama,Mkaguzi Msaidizi Frank
Elophazy,amesema kikosi chake kinakabiliwa na
changamoto za mawasiliano na miundo mbinu isiyo rafiki ya uokozi pindi matukio ya moto yanapotokea.
changamoto za mawasiliano na miundo mbinu isiyo rafiki ya uokozi pindi matukio ya moto yanapotokea.
Wilaya
ya Kahama,imeelezwa kukua kasi,ambapo ina Halmashauri tatu za;Msalala na Ushetu
sambamba na Mji ambapo ndipo yalipo Makao Makuu ya Jeshi hilo kwa wilaya ya
Kahama,huku kukiwa na gari moja kwa ajili ya uzimaji moto,kwa halmashauri zote
tatu,anaandika
Lutufyo Kanyenye.
Elophazy
alikiri kutokana na kukua kwa Mji wa Kahama,kumesababisha kuwepo kwa matukio mengi ya moto tofauti za miaka ya
nyuma,ambapo mengine yamesababishwa na miundo mbinu ya awali ya utandikaji
nyaya za umeme majumbani kuchoka.
Amefafanua
miundo mbinu hiyo ya awali,inashindwa kukabiliana na nishati ya umeme,yenye nguvu kutoka Mgodini
Buzwagi,tofauti na ule wa awali,na kubainisha tatizo hilo limeishapata ufumbuzi
baada ya kuketi na watu wa Tanesco,ambao wanahamasisha wateja wao kubadili na
kuweka miundo mbinu imara.
Mkaguzi
msaidizi huyo,anasema licha ya umbali
katika Halmashauri mbili za Ushetu na Msalala,pindi yatokeapo matukio ya moto.Kwa
upande wa Mji,hukumbana na changamoto ya ujenzi holela wa nyumba za makazi na
biashara,zilizo kikwazo cha kukabili kwa wakati tukio la moto.
Amezidi
kubainisha kwamba ukubwa wa eneo wanalostahili kutoa huduma hiyo,limesababisha
kutokidhi uzimaji moto kwa wakati kutokana na gari wanalomiliki kutokuwa na
ujazo mkubwa wa maji,hivyo kulazimika kuomba kuongezewa lingine lenye ujazo
zaidi.
Anasema,“Kamishina
alipofanya ziara mkoani kwetu,tuliwasilisha maombi ya kuongezewa gari
kubwa,tumepatiwa gari lenye uwezo mkubwa wa kubeba kiasi cha lita 18,000
tofauti la lile la awali ambalo lililokuwa likibeba lita 4000,ama lile la
Buzwagi tuliliomba kuongezewa nguvu ambalo nalo lilikuwa na ujazo wa lita 6000.”
“….lakini
changamoto iliyopo gari hilo linahitaji matengenezo makubwa yanayogharimu Shilingi
Milioni 14.5,ambazo tunalazimika kuzipata kwa michango ya wadau,kibali tumepatiwa kutoka
ofisi nya mkuu wa wilaya,tunaomba wafanyabiashara na jamii nzima ituunge mkono
kufanikisha matengenezo,”alisema
Elophazy.
Wilaya
ya Kahama kwa mwaka jana ilikuwa na matukio ya moto 30 huku ya uokozi yakiwa manne,kwa
kipindi Januari hadi April 18,kulikuwa na matukio ya moto 19 na uokozi 12,jambo lilisababisha kuombwa kwa
gari hilo ili kuongezea nguvu yaliyopo.
KUONA VIDEO MPYA BOFYA HAPA CHINI