BARAZA la Madiwani la Halmashauri ya Msalala
Wilaya ya Kahama,Mkoani Shinyanga limewatimua kazi watumishi wake wa
watano wa idara mbalimbali,kutokana na makosa tofauti tofauti,akiwemo muuguzi aliyempiga makofi mgonjwa.
Maamuzi hayo yamefikiwa kutokana na Baraza hilo,kujigeuza
kamati ya nidhamu,kuketi na kupitia taarifa za uchunguzi za watumishi
mbalimbali baada ya kubaini mapungufu ya kinidhamu,kisha kuchukua maaamuzi hayo
kwa mujibu wa kanuni za utumishi wa umma za mwaka 2003.
Akitangaza maamuzi hayo yaliyobarikiwa na
madiwani hao,Mwenyekiti wa Halmashauri ya Msalala,Mibako Mabubu,alisema katika
kikao cha kamati ya nidhamu ya madiwani kilipokea mashauri nane na kujadiliwa,ambapo
walibaini upungufu huo wa nidhamu,na kuchukua maamuzi hayo sambamba na kumvua
madaraka mtumishi mmoja na kutoa onyo kwa wengine watatu.
Alisema maamuzi hayo yametokana baada ya kubaini
ukosefu wa nidhamu kazini sambamba na utoro kwa watumishi hivyo kuwataka watumishi
wabadilike nakuongeza kuwa kama mfanyakzi ambae hatakwenda na kasi ya awamu ya
tano ni bora akaacha kazi mapema, kabla baraza halijamjadili na kumchukulia
hatua za kisheria.
Mwenyekiti huyo aliwataja waliofukuzwa kazi kuwa
ni Joyce Makewa,ambaye ni Ofisa Muuguzi msaidizi wa daraja la
pili,aliyechukuliwa maamuzi hayo baada kumpiga makofi mgonjwa huku akiwa
ameitumikia halmashauri hiyo kwa kipindi cha miezi 13.
Mabubu alimtaja mwingine kuwa ni Elikana Silasi Masota, ambae alikuwa
na cheo cha Afisa uvuvi Msaadizi,ambae alikaa katika kituo chake cha kazi mwa
muda wa miezi 40 nakubainika kuwa na utoro wa siku 70 hali ambayo kamati
iliazia mtumishi huyo kufukuzwa kazi.
Aliwataja watumishi wengine waliofukuzwa kuwa ni
Edward Lotta ambae ni afisa wa wanyama pori daraja la pili ambae alikaa katika
kituo chake cha kazi kwa muda wa miezi 13 huku akibainika kuwa na utoro wa siku
75,pia Maximilian Kasongo alikuwa mtumishi wa idara ya afya aliyekaa katika
kituo chake cha kazi kwa muda wa miaka 8 huku akibainika kuwa na utoro wa siku
115.
Mtumishi mwingine aliyetimuliwa ni Wencesilaus
Charles, Mhandishi wa ujenzi daraja la pili aliyekaa katika kituo chake cha
kazi miezi 14 alikufukwa kazi kwa kosa la utoro wa siku150.
Aidha alimtaja, Ester Nduguru ambae alikuwa
mhudumu wa afya aliyekaa katika kituo chake cha kazi kwa miezi 20 alibainika
kuwa na utoro wa siku tatu ambao sii zaidi ya siku tano kisheria hakukutwa na
hatia na kamati imeridhia kurudishwa kwenye orodha ya malipo ya mishahara.
Hata hivyo aliyekuwa Mkuu wa Idara ya Ujenzi
katika Halmashauri;Pharles Ngeleja,amevuliwa wadhifa baada ya kubainika
kuidhinisha mitambo ya ujenzi kwenda nje ya mkoa bila idhini ya Mkurugenzi huku akiwa
ameitumikia miezi 15,kitendo ambacho ni kutumia madaraka yake vibaya lakini
ataendelea na kazi yake ya uhandisi.
Mtumishi wa mwisho alisema kuwa ni Syvester
Machiya ambae alikuwa ni fundi msanifu ujenzi mkuu aliyekaa kazini ndani ya
miaka 4 na alikuwa akitumia bila idhini ya mamlaka husika mali ya mwajiri wake
hivyo kamati ilianzia kumtoa hatiani mtumishi huyo.
Mabubu alimuonya Mkurugenzi Mtendaji wa
Halmashauri hiyo,Simon Berege,kusimamia mamlaka yake vema kwa kuchukua hatua kali kwa kila mtumishi
atakaekwenda kinyume na taaraibu za kazi,vinginevyo asipochukua hatua za
kisheria kwa watumishi hao, Baraza litaanza na mkurugenzi kisha kwenda kwa
watumishi wengine.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya
Msalala,Simon Berege,anatoa onyo kwa watumishi kuzingatia nidhamu kazini na
kuzingatia uwajibikaji na hata sita kumchukulia hatua yeyote atakayekiuka
misingi yake ya kazi.
Anasema “Serikali ya awamu ya tano inazingatia
uwajibikaji,nami nitamuwajibisha kwa hatua kali za kitumishi yeyote
atakayekiuka misingi yake ya kazi sintongoja Baraza ambalo mchakato wake ni
mrefu kufikia maamuzi haya.”