Sunday, October 30, 2016

POLISI YAMZUIA MAALIM SEIF,YAMLINDA LIPUMBA.

BOFYA HAPA CHINI KUONA MAAJABU YA LEO



JESHI la Polisi limedhibiti mkutano mkuu maalumu wa Chama cha Wananchi “CUF”ambao ungehudhuriwa na
 Katibu Mkuu wa chama hicho, Maalim Seif Sharif Hamad mjini Tanga.

Jeshi hilo likidhibiti mkutano huo jana,limeshiriki kikamilifu kumlinda Mwenyekiti anayetambuliwa na Msajili wa Vyama vya Siasa, Profesa Ibrahim Haruna Lipumba,wakati akifanya usafi soko la Buguruni. 

Lipumba aliungana na Watanzania katika kutekeleza agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt.John Pombe Magufuli,kufanya kazi ya usafi,inayotekelezeka siku ya  Jumamosi ya kila mwisho wa mwezi.

Kitendo hicho cha Mwenyekiti huyo anayetambulika na Msajiri wa Vyama vya Siasa,kimetetewa na  Msemaji wa CUF,wa kambi inayomkubali Profesa Lipumba,Abdul Kambaya,kwa kusema hakuna jambo la ajabu, kwa Kiongozi wa Chama cha Upinzani,kufanya usafi huku akilindwa.



Wakati Lipumba akiunga jitihada za Rais Magufuli kwa kuwepo utamaduni wa kusafisha mazingira,chini ya uangalizi wa Jeshi la Polisi,mapema jana, polisi mjini Tanga ilizuia mkutano uliopangwa kuhudhuriwa na Maalim Seif.

Katika mkutano huo ambao ulikuwa na agenda ya  kujadili madiwani 12, waliopigana wiki iliyopita katika ofisi za chama hicho wilayani humo, baada ya kugawanyika kuhusu uamuzi wa wenzao kuhudhuria baraza la madiwani wa jiji hilo Oktoba 12.

Taarifa ya jeshi hilo ilidai kuzuiwa kwa mkutano huo ni kutokana na tisho la uvunjifu wa amani na kuwapo kwa makundi mawili yanayozozana. Mkutano huo ulipangwa kufanyika katika Hoteli ya Mkonge mjini Tanga.

Pia, taarifa iliyotolewa na Mkuu wa Polisi Wilaya ya Tanga, Idd Abdallah ilisema ukumbi ambao mkutano huo ungefanyika ni mdogo kutokana na wingi wa wanachama.

 “Ukumbi uliopangwa kufanyika kwa mkutano huo ni mdogo na ikumbukwe kuwa wiki iliyopita mkutano wa chama hicho ngazi ya wilaya ulivunjika kutokana na vurugu,” alisema

Akizungumzia sakata hilo, Mwenyekiti wa CUF wa wilaya hiyo, Rashid Jumbe alisema hata kama jeshi hilo limezuia mkutano huo, lengo la chama kuwajadili madiwani hao liko palepale. 

Alisema kamati ya utendaji imependekeza madiwani saba,kati ya 12 wafukuzwe uanachama kutokana na kukiuka msimamo wa chama,huku watano wakibaki chini ya uchunguzi.

Amebainisha kwamba katika fagio hilo,Mbunge (Mussa Mbaruku),hatasalimika kwani alishiriki kikamilifu,pamoja na Naibu Meya (Mohamed Aniu).

“…. kwa sasa tunafanya utaratibu na jeshi la polisi kutekeleza masharti na vigezo wanavyotaka ili kuufanya mkutano huo tena,” alisema.

KUONA VIDEO MPYA BOFYA HAPA CHINI