MAHAKAMA Kuu Kanda ya Shinyanga jana imetupilia mbali Shauri alilofungua
aliyekuwa Mgombea Ubunge Jimbo la Kahama Mjini,James Lembeli,kupitia
tiketi ya Chadema ya kuomba kutenguliwa Matokeo ya uchaguzi katika Jimbo
hilo kwa madai kuna taratibu zilikiukwa na mshindi katika Uchaguzi
huo,Jumanne Kishimba.
Lembeli katika kesi hiyo namba 1/2015 iliyokuwa ikisikilizwa na Jaji Moses Mzuna,aliyofungua katika Mahakama Kuu,Kanda ya Shinyanga Mwezi Novemba mwaka jana, ilikuwa ikimtuhumu Mbunge wa Jimbo la Kahama Mjini, Kishimba kutoa Rushwa katika Kampeni zake Ubunge, kutotendewa haki na msimamizi wa Uchaguzi ambaye ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Kahama.
Pia sababu nyingine ilikuwa ni kukamatwa kwa watu ambao alidai kuwa walikuwa ni Mawakala wake 11 kati ya 14 na kufunguliwa mashitaka katika Mahakama ya Wilaya ya Kahama kujibu tuhuma za kutaka kuvuruga shughuli nzima za Uchaguzi katika kipindi hicho ambao ilikuwa ukifanyika nchi nzima.
Akitoa hukumu hiyo katika Mahakama kuu Kanda ya Shinyanga iliyofanyika katika Wilaya ya Kahama Jaji Moses Mzuna alisema kuwa matokeo ya Uchaguzi wa Ubunge wa Jimbo la Kahama Mjini hayawezi kutenguliwa kutoka na Ushahidi wa upande wa mleta maombi James Lembeli kutojitosheleza.
Mzuna aliiambia Mahakama kuwa ushahidi wa Mashahidi wa Mleta maombi huyo hayakuwa na mashiko ya kuweza kuifanya Mahakama kuweza kutengua matokeo hayo kwani haukulingana na Madai yaliyowakishwa Mahakamani hapo na Mleta maombi kwa kushindwa kutoa uthibitisho wa Madai yake.
Jaji huyo aliendelea kuiambia Mahakama kuwa unapopeleka Madai Mahakamani kwa kesi kama hizi za uchaguzi ambazo uzito wake haulingani na kesi za kawaida lazima mdai kupaswa kuwakilisha madai yake yakiambatana na Ushahidi wa vithibitisho vya Maandishi.
Mzuna alisema kuwa kulingana na mwenendo wa kesi ilivyokuwa ilionekana kuwa Malalamikaji alipaswa kuwakisha awali pingamizi lake katika ngazi husika za uchaguzi hasa baada ya kupewa taarifa za kuwepo kwa vitendo vya Rushwa katika vituo vya uchaguzi na sii kukimbilia Mahakamani kabla
Aidha katika hukumu hiyo iliyodumu kwa saa nne Jaji mzuna alisema kuwa katika suala la utoaji wa Rushwa za masufuria kilichoelwa katika hati ya madai ni tofauti na ushahidili uliotolewa kwa upande wa Mtoa maombi ambapo awali alieleza kutolifahamu jina la kikundi ambacho kilipewa huku katika mwenendo wa kesi kitajwa jina Amani.
Jaji huyo alisema kuwa katika kesi hizo za uchaguzi, Mahakama haiwezi kutengua kesi hizo za Wagombea kwa ajili ya kufurahisha watu kwani katika jamii inayoamini msuala ya Demokrasia uchaguzi ni kitu Adimu sana na kitakatifu na kinachotumia gharama nyingi hivyo maamuzi yanayotolewa na watu lazima yaheshimiwe.
Katika kesi hiyo upande wa mashitaka ulikuwa ukiongozwa Mwanasheria Mpale Mpoki huku upande wa utetezi ukiwa ukiwakilishwa na Wanasheria Wawili ambao ni Anthon Asimile, Denis Kahangwa ambao walimwakilisha Jumanne Kishimba (CCM) huku upande wa Serikali ukiongozwa Kastus Ndaiyoba pamoja na Upendo Malulu.
Akizungumza na Wananchi pamoja na Wanachama wa Chadema muda mfupi baada ya kutoka Mahakamani, aliwataka Wananchi kuwa watulivu kwani kitendo kilichofwa na Mahakanama hiyo sio cha haki na kuongeza kuwa atakaa na Mwanasheria wake Mpale Mpoki ili kuliangalia upya suala hilo na kuangalia jinsi ya kufanya.
KUONA VIDEO MPYA BOFYA HAPA CHINI