SAKATA la Wahisani kusitisha misaada
Tanzania,limeingia katika sura mpya baada ya baadhi ya Wajumbe wa Baraza la
Wawakilishi,kujitokeza na kukishutumu Chama cha Wananchi (CUF) pamoja na
viongozi wao kwa kukosa uzalendo kutokana na kauli zao za kuunga mkono,maamuzi
hayo ya wahisani.
Shutuma hizo zilitolewa na
Mwakilishi wa kuteuliwa kutoka katika chama cha Ada-Tadea, Juma Ali Khatib,wakati
alipokuwa akichangia hotuba ya Rais wa Zanzibar kwenye kikao cha baraza hilo.
Juma Ali Khatibu, ambaye aligombea
urais wa Zanzibar katika Uchaguzi Mkuu wa marudio, alisema, viongozi wa CUF
wameonesha udhaifu mkubwa wa kukosa uzalendo kwa kitendo chao cha kuunga mkono
nchi washiriki wa maendeleo kususa misaada kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania.
Alisema, Zanzibar ni nchi yenye
kufuata katiba yake kwa hiyo ilikuwa na mamlaka kamili kupitia Tume ya Uchaguzi
ya Zanzibar (ZEC), kuitisha uchaguzi wa marudio baada ya kuufuta wa Oktoba 25,
mwaka jana.
Mwakilishi huyo alisema chama chake
kiliamua kuingia katika uchaguzi wa marudio wa Machi 20 kwa sababu umeitishwa
na chombo halali kwa mujibu wa katiba, chenye majukumu ya kusimamia uchaguzi
kikiwa hakiingiliwi na mtu yeyote.
Nae Mwakilishi wa Jimbo la Mfenesini
, Machano Othman Said, alisema kitendo cha viongozi wa Cuf kuunga mkono nchi
washiriki wa maendeleo kususa kutoa misaada kwa Tanzania hakikubaliki hata
kidogo kikionesha udhaifu mkubwa wa viongozi hao katika uzalendo wa nchi.
KUONA VIDEO MPYA BOFYA HAPA CHINI