BARAZA
Kuu la Waislaam nchini (Bakwata) kwa kushirikiana na Shia wameikabidhi Serikali
msaada wa madawati 500,ili kusaidia upungufu uliopo nchini wa madawati
kwa shule za msingi na sekondari.
Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania,
Abubakar Bin Zuberi, amesema katika hafla ya kukabidhi madawati hayo kuwa katika msaada hawaangalii suala la dini,bali
kinachoangaliwa ni watakaokalia madawati hayo kuwa ni Watanzania.
Mufti
Zuberi amesema kuwa wamechangia dawati hizo ili kuunga jitihada za Serikali katika kutekeleza kauli mbiu ya elimu bure,kuanzia chekechea hadi kidato cha nne,na imani yao kubwa msaada huo utasaidia kwa kiwango chake watoto wa Watanzania kupata Elimu stahiki.
Amesema
kuwa wataendelea kushawishi waislaam katika kuendelea kuchangia elimu
ili watoto wapate elimu iliyo bora kwa kuwa serikali pekee yake haiwezi
kutatua changamoto zote za elimu.
Mwenyekiti
wa SHIA, Azim Dewj amesema kuwa amepeleka msaada huo katika bakwata
ikiwa ni kuonyesha umoja na jinsi ya kusaidia serikali katika upande wa
elimu.
Amesema
kuwa ataendelea kushawishi matajiri wenzake kuangalia namna
watakavyosaidia katika sekta ya elimu upande wa madawati kuwa kila mwaka
kuweza kuchangia madawati 1000.
Waziri
wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk. Hussein Mwinyi akizungumza kwa
niaba ya Waziri Mkuu amesema kuwa msaada wa madawati hayo ni mkubwa
kutokana na changamoto iliyopo mbele yao.
Amesema
kuwa idadi ya wanafunzi wa darasa la kwanza kuandikishwa umeongezeka
kutokana na mpango wa elimu bure hivyo serikali kupata madawati ni
jambo la furaha na kuwataka wadau wengine kujitokeza kuchangia madawati
kutokana na mahitaji kuwa makubwa.
KUONA VIDEO MPYA BOFYA HAPA CHINI