BAADA
ya kupita chache tangu kuibuka kwa kashfa ya rushwa miongoni mwa wajumbe wa
Kamati za Kudumu za Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Taasisi ya Kuzuia
na Kupambana na Rushwa (Takukuru) imemuita Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe,
kumhoji.
Mbunge huyo machachari na kipenzi za vijana wengi nchini,Zitto pamoja na mwenzake wa Jimbo la Nzega Mjini,Hussein Bashe, ambao ni wajumbe wa Kamati ya Huduma za Jamii, walichukua maamuzi mazito muda mfupi baada ya taarifa za kashfa hiyo, kumuandikia barua Spika wa Bunge, Job Ndugai kujiondoa kwenye nafasi zao.
Wabunge
hao katika barua yao walijieleza kujiondoa katika Kamati hiyo ili kupisha
uchunguzi dhidi ya tuhuma hizo.
Zitto alithibitisha kupata wito kutoka makao makuu ya Takukuru kupitia ofisi za bunge,ili kuhojiwa juu ya sakata hilo, na kupongeza kwa hatua hiyo iliyochukuliwa na Taasisi hiyo, iliyoonesha uwajibikaji unaoenda na wakati.
Alisema
pindi vyombo vya Serikali vitakuwa makini kushughulikia tuhuma zote
zinazoelekezwa kwa wanasiasa na watumishi wengine wa umma, itasaidia kuongeza
uwajibikaji na kupunguza uzushi kwa wananchi.
“Nasikia pia Bashe ameitwa. Nafurahi wito wetu wa uchunguzi umechukuliwa kwa uzito unaostahili, nasi tutatoa ushirikiano unastahiki kwa vyombo vya uchunguzi ili kumaliza zoezi hili kwa haraka na kwa ufanisi,” alisema Zitto.
Alipotafutwa Bashe ili kupata ukweli wa kuitwa kwake, ingawa hakutimiza ahadi yake, alisema,hayupo katika eneo muafaka kuzungumzia suala hilo japo taarifa zinaeleza ni miongoni mwa wanahojiwa na Takukuru sambamba na watendaji wa mashirika yaliyotajwa kuhusika kutoa rushwa.
Watendaji
hao wa mashirika walidaiwa kutoa rushwa ili kubadili maoni ya wajumbe juu ya
utendaji wao,na tayari wabunge hao wawili miongoni mwa wajumbe wa Kamati hiyo
walithibitika kuitwa na Takukuru.
Tuhuma hizo zimekwenda sambamba na Ndugai kuwaondoa wenyeviti wa kamati za Ardhi, Maliasili na Utalii; Nishati Madini; Uwekezaji na Mitaji ya Umma huku ile ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) na Huduma na Maendeleo ya Jamii lakini akisema ni uhamisho wa kawaida.
Mkurugenzi Mkuu wa Taakukuru, Valentino Mlowola, bila kuingilia uchunguzi unaoendelea alithibitisha kuwaita wabunge hao na watendaji wa mashirika kuhojiwa na taarifa kamili itatolewa pindi uchunguzi utakapokamilika. KUONA VIDEO MPYA BOFYA HAPA CHINI