Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Magufuli,amekabidhiwa ripoti tano na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG)Mussa Assad, ambazo anaweza kuzitumia kama kitendea kazi.
Ripoti hizo pindi akizitumia ipasavyo zitamuwezesha kutekeleza kauli mbiu yake ya kutumbua majipu,kwa uhakika zaidi kwa kuendelea kuibua uozo zaidi ambao umebainika katika ukaguzi wa CAG,
Rais Magufuli tangu ameingia madarakani amekuwa akiibua uozo kwenye taasisi za
Serikali, kusimamisha na kutengua uteuzi wa watumishi wa umma
wanaojihusisha na ufisadi na wakati fulani amekuwa akiitaja ripoti
iliyopita ya CAG kuwa ndiyo iliyoanika uozo anaofanyia kazi.
Jana,
“mtumbua majipu” huyo alikabidhiwa ripoti ya kwanza ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) tangu
aapishwe kuwa Rais Novemba 5 mwaka jana na sasa ana kitendea kazi rasmi
cha kufanyia kazi.
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG)Assad, alimkabidhi Rais Magufuli
taarifa ya ukaguzi wa hesabu za Serikali ikiwa ni kwa mujibu wa Katiba
inayomtaka akabidhi ripoti hizo kwa Rais kabla ya mwisho wa mwezi Machi.
Taarifa iliyotolewa na Gerson Msigwa, kaimu mkurugenzi wa
mawasiliano – Ikulu, Rais Magufuli, ambaye aliwaomba wabunge kumpa
ushirikiano katika kutekeleza kazi za wananchi wakati akizindua Bunge
Novemba 20, atazikabidhi ripoti hizo kwenye chombo hicho ndani ya siku
saba za mwanzo za Mkutano wa Tatu wa Bunge la Kumi na Moja utakaofanyika
mjini Dodoma kuanzia Aprili 19.
“Rais Magufuli amempongeza CAG
na timu yake kwa kuandaa taarifa hiyo na ametoa wito kwa chombo hicho
kuendelea kufanya kazi kwa uhuru na ufanisi. Ameahidi kuwa serikali
itatoa ushirikiano wa kutosha kufanikisha kazi zake,” inasema taarifa
hiyo.
KUONA VIDEO MPYA BOFYA HAPA CHINI