Tuesday, December 2, 2014

“SUGAR DADDY,MOMY” KAHAMA WAONYWA

BOFYA HAPA CHINI KUONA MAAJABU YA LEO

WANAFUNZI wa darasa la kwanza katika Shule ya Msingi Lushelo Kata ya Kinamapula;Alfred Amos na Marco Robart wakionyesha umahiri mkubwa wa kucheza muziki kwenye kilele cha Maadhimisho ya Ukimwi.
 WANAUME wenye umri mkubwa “Sugar Daddy” sambamba na wanawake wenye umri huo “Sugar Mummy”wameonywa kuondokana na tabia za ufuska ambazo zimechangia kwa kiwango kikubwa maambukizi ya Ukimwi kwa
Vijana.
MRATIBU wa Shughuli za Maabara katika Halmashauri ya Ushetu wilayani Kahama,Riziki Kweka akiendelea na shughuli za upimaji na ushauri wa maradhi ya UKIMWI hapa akichukua damu tayari kwa vipimo ili kubaini kama imeathirika ama haijaathirika na Virusi vya UKIMWI.

Hali hiyo ilibainishwa katika maadhimisho ya kumbukumbu za Ukimwi Duniani zilizofanyika kiwilaya kata ya Kinamapula katika Halmashauri ya wilaya ya Ushetu na Diwani wa Kata ya Mpunze,Benedicto Mabuga ambapo alisema takwimu zinaonyesha vijana wengi kuathirika na maradhi hayo.

Alisema hali halisi inaonyesha watu wenye umri mkubwa kufanya mapenzi na wasichana wa umri mdogo huku bibi vizee nao kutaka mapenzi na wavulana wadogo hali ambayo imeathiri vijana wengi kuwa na maambukizi ya ugonjwa huo
DIWANI wa Kata ya Mpunze Benedicto Bundala akikabidhi zawadi kwa ajili ya watoto wanaoishi katika mazingira magumu baada ya kufiwa na wazazi wao.
 

Diwani Mabuga alikuwa mgeni rasmi kwa niaba ya Mkuu wa wilaya ya Kahama,Benson Mpesya alisema takwimu zinaonyesha vijana kati ya miaka 15 hadi 49 idadi kubwa wameambukizwa virusi vya Ukimwi hali inayoonyesha kuwepo kwa mwingiliano mbaya wa kimapenzi baina yao na watu wazima.


Hata hivyo Mabuga amesema pamoja na changamoto hiyo halmashauri yake ya Ushetu ambayo ni moja ya halmashauri zingine mbili za mji na Msalala zilizopo wilayani Kahama imeweka mikakati mbalimbali ya kukabiliana na janga hilo
WASANII wa Kahama Medical Culture Troupe walitoa burudani katika maadhimisho hayo.



Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Ushetu Anna Ngongi alisema Jumla ya watu 5200 katika Halmashauri hiyo wanaishi na virusi vya ukimwi na tayari wamejiunga na huduma ya  kliniki ya tiba na mafunzo huku 2800 kati yao  wameanza kutumia dawa ya kupunguza makali ya ugonjwa wa ukimwi



Katika taarifa ya Halmashauri hiyo juu ya maambukizi ya Ukimwi, Ngongi alisema idadi hiyo ni kubwa kwa kuwa ni sawa na asilimia 5 tofauti ya alama moja ya takwimu za kitaifa za asilimia 5.1 hali ambayo jamii inatakiwa kushilikiana kuweka nguvu za pamoja kupambana na janga hilo

KUONA VIDEO MPYA BOFYA HAPA CHINI