BOFYA HAPA CHINI KUONA MAAJABU YA LEO
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhmGnlGKofOAsUNWCXRxnKQFr6MBeHOOdr3ze_gipbvY5vwCHBWhdV08xe-HNOnMN1KuKQm0fawB9a0_dRWh0mlFEJIdkQY9x9kQ8YPj4zrg3hYcB2pnYDP0sAJSsn7jBVTAP3C4QHQcGI/s1600/DSCN0443.JPG) |
MHUDUMU wa Afya wa Zahanati ya kijiji cha Segese katika Halmashauri ya wilaya ya Msalala,Michael Natoboki akimpatia chanjo ya Vitamini A,mtoto Joseph Ntobi mwenye mwaka mmoja na mwezi mmoja. |
MKOA wa Shinyanga unatarajia kuwafikia
na kuwapatia chanjo watoto 737,000 katika zoezi la chanjo linaloendelea nchi nzima.
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjzS5UlA9HB-NlAp-D6SW0wUn5zMGSVlWb1CVz0rHnbNrvOjUpAuUWn54hIV0ISwyxo122xiq46baFusx6o8XzXMQfm2IUsAtj7EJ-zyiMtPggYdX0z8FtoRxdXh0UL-SLL64g2yO4VQl4/s1600/DSCN0376.JPG) |
MTOTO Benedicto Ruta akipatiwa matone ya Vitamini A na Mhudumu wa Afya wa Zahanati ya kijiji cha Segese katika Halmashauri ya wilaya ya Msalala,Michael Natoboki,katika viwanja vya Shule ya Msingi Segese A,iliyopo Kata ya Segese katika Halmashauri ya wilaya ya Msalala. |
Hayo yalielezwa na Mganga Mkuu wa Mkoa
wa Shinyanga Ntuli Kapologwe,ambapo alisema katika zoezi hilo linaloendelea nchi
nzima mkoa wa Shinyanga imejiwekea malengo ya kuwafikia na kuwapatia chanjo
watoto hao.
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhajp_sc8eNR__Os6UB4knQSp_zHDRYXg7KApDJTc5LwIbFjmeiRx8JByojLhSSxnABI0MbCCehtk9dBgTM_8TvRQE5H604Y6Hl0yGfgZfrzGDe2iXkdjvDWbzzVY_cJRhznqRYXiOAc_g/s1600/DSCN0378.JPG) |
NESI wa Zahanati ya Kijiji cha Segese katika Halmashauri ya wilaya ya Msalala,Elinami Ulomi akimpatia chanjo mtoto Benedicto Ruta katika viwanja vya Shule ya Msingi Segese A.
|
|
| |
NESI wa Zahanati ya Kijiji cha Segese katika
Halmashauri ya wilaya ya Msalala,Elinami Ulomi akimpatia chanjo mwanafunzi wa kidato cha kwanza Shule ya Sekondari ya Mwalimu Nyerere,Irine Ruvulahindi katika viwanja vya Shule ya Msingi Segese A. |
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhJjEmtM1tzIgoNN69IQPqKHjkWyRJn2ymkIsb1YFyLGAoRnhOMbLiw-oNTSRgcEXyVNxod3DwKR1B0_5mz7llgB4vIe5mJsrlQ_Ic3jpYCkJ9_TKTwjs5x9_wGeQ51RSetwZGu6d3mLKY/s1600/DSCN0440.JPG) |
WATOTO wa kijiji cha Segese walijitokeza wenyewe pasipo kusindikizwa na wazazi ama walezi.
Kapologwe alieleza katika zoezi hilo
linalofanyika nchi nzima limelenga kuwapatia chanjo mbalimbali watoto wa kuanzia miezi sita
mpaka chini ya miaka 15,ambapo watapatiwa chanjo za Rubella na
Surua ikiwemo vitamini A,ili kuzuia magonjwa ya Surua, moyo na Minyoo.
|
Hivyo aliwakumbusha wazazi kujitokeza kuwapeleka watoto wao katika
vituo vilivyoteuliwa kwa ajili ya kutolea chanjo.
KUONA VIDEO MPYA BOFYA HAPA CHINI